MSAJILI WA NGOS ATEMBELEA TAASISI YA SERIS KATIKA KIKAO KILICHOFANYIKA MAKAO MAKUU YA SERIS FOUNDATION JIJINI DAR ES SALAAM.

Msajili Msaidizi wa NGO za Halmashauri ya Ilala, Bi. Mwanaisha Boffu, atembelea Seris Foundation leo tarehe 12 oktoba 2024 katika makao makuu yake apa Samora Avenue, Holland House na kupongeza kazi ambazo imekuwa ikifanya tangu kuanza kwake kazi mwezi Mei 2023. Katika kikao hicho, anaeleza namna ambavyo serikali inafanya kazi na NGO na anapongeza Seris Foundation kwa jinsi inavyoshirikisha Serikali katika mipango na kazi zake mbalimbali. Hata hivyo, Msajili Msaidizi anasisitiza umuhimu wa utoaji wa taarifa, kwani hizo ndizo zinazoonesha uhai wa taasisi husika. Mwishoni, anawatakia wafanyakazi wote wa Seris Foundation utekelezaji mzuri wa mipango mbalimbali waliojiwekea. Wajumbe wa Seris Foundation wanamshukuru Msajili kwa kuwatembelea na kusikiliza kazi walizokwisha kufanya na zile wanazopanga kufanya.