HITIMISHO LA WARSHA YA ADVANCED ENGINEERING SOFTWARE, LEADERSHIP, AND ENTREPRENEURSHIP
Leo tumefikia hitimisho la siku ya warsha ya kipekee iliyofanyika Landmark Hotel - Riverside, Ubungo, Dar es Salaam. Siku ya leo imekuwa ya mafanikio makubwa, tukiangazia mafunzo maalum juu ya "Flood Risk Assessment using RAS-2025 - Integrating Hydraulic Modeling for Flood Mitigation" yaliyotolewa na mkufunzi mahiri, Eng. Ramadhan Twaha Mafunzo haya yamelenga kuwajengea washiriki uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa kutathmini hatari za mafuriko, kuboresha mifumo ya mifano ya kihaidroliki, na kuimarisha juhudi za kupunguza athari za mafuriko. Tunatoa shukrani za dhati kwa wote walioshiriki, hasa mkufunzi wetu Eng. Twaha kwa maarifa na weledi wake. Tunapohitimisha, tunahimiza washiriki wote kutumia maarifa haya kwa vitendo ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya uhandisi na uongozi. Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii na tovuti yetu kwa taarifa zaidi kuhusu mafunzo na programu zetu zijazo.