SERIS FOUNDATION YATOA MSAADA WA VIFAA KWA WATOTO WACHANGA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
TAASISI ya SERIS (Seris Foundation) yenye makao makuu yake Ilala, Jijini Dar es Salaam leo Juni 16, imetembelea na kutoa msaada wa vifaa kwa Watoto Wachanga waliozaliwa usiku wa kuamkia leo Juni 16 katika Hospitali Mkoa ya Rufaa ya Amana, ambapo Tanzania na Afrika kwa ujumla inaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika.
Awali akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali hiyo, Ofisa Muuguzi kiongozi wa Hospitali ya Amana, Vicent Sinkamba ameishukuru taasisi ya SERIS kwa vifaa hivyo, huku akiendelea kuomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia mahitaji muhimu.