SERIS FOUNDATION YADHAMINI MRADI WA KUWAWEZESHA VIJANA KATIKA MAENDELEO YA TAALUMA NA AFYA YA AKILI

TAASISI ya SERIS ilikuwa miongoni mwa wadhamini na washirika wa Mradi wa Ndoto. Viongozi wa shirika hilo chini ya Mkurugenzi Mtendaji CPA Deborah Wami walikuwepo kusaidia shughuli ya kuongoza shuleni iliyofanyika tarehe 18 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam.
 Mradi huu uko chini ya rais Bi. Ashely Andeta na waratibu wengine kutoka shule za kimataifa. Mradi huu unalenga kuwawezesha vijana katika maendeleo ya taaluma na afya ya akili.