SERIS FOUNDATION KUSHIRIKI KWENYE KILELE CHA MATEMBEZI YA HISANI AMBAYO YALIKUA NA LENGO LA KUSAIDIA WATOTO WANAOZALIWA KABLA YA WAKATI
TAASISI ya SERIS imekuwa miongoni mwa taasisi zilishoriki kwenye kilele cha matembezi ya hisani tarehe 10 agosti, 2024 ambayo yalikuwa na lengo la kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati pamoja na ujenzi wa wodi kwa watoto hao ndani ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke .Matembezi hayo yalianzia katika viwanja vya mwembe yanga, Temeke na kuishia katika viwanja hivyo kwa sherehe fupi pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza.