SERIS FOUNDATION IMESHIRIKI KWENYE MKUTANO WA MWAKA WA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

TAASISI ya SERIS (Seris Foundation) yenye makao makuu yake Ilala, Jijini Dar es Salaam leo tar 20 agosti, 2024, imeshiriki kwenye mkutano wa mwaka wa taasisi zisizo za kiserikali za ndani ya jiji la Dar es salaam iliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Dar es salaam mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya Mh.Edward Mpogolo.Lengo la mkutano ni kuwaita wote pamoja wadau wa maendeleo wa taasisi zisizo za kiserikali na kujadili namna bora ya kuendesha taasisi hizo.