SERIS FOUNDATION IMESHIRIKI KWENYE MKUTANO WA MWAKA WA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

TAASISI ya SERIS (Seris Foundation) yenye makao makuu yake Ilala, Jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, imeshiriki kwenye mkutano wa mwaka wa taasisi zisizo za kiserikali za ndani ya jiji la Dar es salaam iliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Dar es salaam mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa mkoa Mh.Albert Chalamila.Lengo la mkutano ni kuwasisitiza juu ya kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2025, utawala bora pamoja na kufanya kazi na serikali ili kutimiza malengo ya nchi.