Youth in Science and Technology (YST) Summit Imefunguliwa rasmi leo tarehe 2 Juni 2025

YST Summit 2025 imefunguliwa rasmi kwa mafanikio makubwa katika ukumbi wa PSSSF Commercial Complex, Dar es Salaam. Hafla hii imewakutanisha vijana kutoka kote nchini kwa siku nne za mafunzo, ubunifu na majadiliano kuhusu mchango wa vijana katika sayansi na teknolojia.

Ufunguzi ulihudhuriwa na Seris Foundation, ERB, na AQRB, ambapo viongozi walitoa hotuba zenye hamasa kuhusu nafasi ya vijana katika kuleta suluhisho bunifu kwa changamoto za jamii. Ubunifu wa vijana kama Smart Egg Incubator na Bamboo Innovation uliwasilishwa, huku mada muhimu kama madhara ya dawa za kulevya na Work-Life Balance zikijadiliwa na wataalamu.