YOUTH IN SCIENCE AND TECHNOLOGY (YST) SUMMIT SIKU YA HITIMISHO
YST Summit 2025 iliendelea kwa siku ya tatu tarehe 4 Juni 2025 katika ukumbi wa PSSSF Commercial Complex, Dar es Salaam, ambapo washiriki walielekezwa kwenye maudhui ya Professional Practice and Opportunities kwa lengo la kuwapa vijana maarifa ya kujisajili kitaaluma na kufungua milango ya fursa.
Eng. Tereza Laurent kutoka ERB alieleza hatua muhimu katika usajili wa kampuni za ushauri wa kihandisi, akisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu rasmi ili kujenga uaminifu na ufanisi. Mwakilishi kutoka CRB alifafanua mchakato wa usajili kwa wakandarasi, huku AQRB wakitoa miongozo kwa wasanifu majengo na wapimaji gharama kuhusu usajili na maadili ya taaluma.
Ms. Rehema Bashiri, Mkurugenzi Mkuu wa Zumra Microfinance, aliwapa vijana maarifa kuhusu fursa za kifedha kwa startups, akihamasisha ujasiriamali wenye msingi wa kisheria na kifedha imara.
Siku ilihitimishwa kwa hotuba za kuhamasisha kutoka kwa Eng. Benard Kavishe, Msajili wa ERB, na Glory Blasio Emmanuel kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), waliowataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kutumia fursa za taaluma na biashara kwa maendeleo yao na ya taifa kwa ujumla.