SERIS FOUNDATION IKITOA HUDUMA KATIKA ANNUAL ENGINEERS DAY (AED25)

Seris Foundation imepata nafasi ya kipekee kushiriki katika Annual Engineers Day (AED) 2025 Septemba 25–26, tukibeba dhamira ya kuonyesha nguvu ya vijana wabunifu na kugusa maisha ya jamii. Katika maonesho haya, tumewasilisha na kuuza bunifu za vijana wetu – Smart Egg Incubator na Bamboo Briquettes – kama sehemu ya suluhisho za kiteknolojia na nishati safi zinazojibu changamoto za sasa.

Sambamba na hilo, tumeendesha fundraising ya watoto wachanga kupitia mauzo ya Baby Pack, ambapo fedha zote zilizopatikana zitapelekwa kununua mahitaji ya watoto wachanga. Mwaka jana tulifanikisha kuwafikia zaidi ya watoto 27 Hospitali ya Amana, na mwaka huu tutaendelea na safari ya upendo kwa kutembelea watoto wachanga Hospitali ya Mnazi Mmoja mwishoni mwa Novemba 2025.

Zaidi ya maonesho haya, Seris Foundation tulishiriki pia katika Youth in Engineering Forum (YEF) ambapo tuliweza kuhudumia zaidi ya vijana 103, na katika mkutano wa 22 wa siku ya wahandisi nchini AED 2025 Seris Foundation tumetoa huduma kwa zaidi ya wahandisi 350 waliotembelea banda letu.

Tunaamini kila ubunifu wa kijana na kila mchango kutoka kwa wadau ni uwekezaji katika mustakabali wa taifa letu. 

Tunawakaribisha wadau, washirika, na marafiki kuendelea kuungana nasi  kukuza ubunifu, kuwekeza kwenye ndoto za vijana na kuleta tabasamu kwa watoto wachanga