Seris Foundation Yakabidhi Vifaa Tiba kwa Wodi ya Mama na Mtoto Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam tarehe 1 Desemba 2025
Seris Foundation imetoa vifaa tiba kwa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar-es-Salaam tarehe 1 Desemba 2025, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.
Utoaji huu wa vifaa umefanyika kwa ushirikiano kati ya Seris Foundation na Lions Club International ambapo pande hizo mbili zimejumuisha nguvu ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa akina mama na watoto.
Seris Foundation, ambayo inajikita katika kuwawezesha vijana wa fani za sayansi na teknolojia inaendelea kujidhihirisha kama mdau muhimu wa maendeleo ya jamii kupitia miradi ya kimkakati inayoleta tija.Kupitia msaada huu taasisi inalenga kuboresha ustawi wa mama na mtoto pamoja na kuunga mkono jitihada za kitaifa katika kuinua sekta ya afya.